Header Ads

PUMZIKA KWA AMANI KAKA YETU Y.P

 Msanii 'YP' toka kundi la TMK Wanaume Family amefariki jana usiku katika hospitali ya TMK ambako alikuwa akisumbiliwa na kifua kwa muda mrefu lakini hali ilikuwa mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.  Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fela amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Msiba wa msanii huyo uko Keko nyumbani kwa baba yake. Said Fella amesema Marehemu ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambikile alifanya vizuri na msanii mwingine Y Dash na nyimbo kama 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family.
YP akiwa na chama lake Chege na Temba Kutoka TMK
YP akiwa na Aslay pamoja na Stiko enzi za Uhai wake

No comments:

Powered by Blogger.