Mubwa na wanawe & High Class Look Yatoa Msaada kwa Watoto yatima Mbagala
Mkubwa Fella akikabidhi kiroba cha Sembe kwa Bi Hawa Mmiliki wa Kituo cha watoto yatima Hazina kilichopo Mbagala maji Matitu. |
Picha ya Pamoja na Watoto hao |
Vijana wa Yamoto Band Wakitoa Burudani kwa watoto hao. |
Kabla ya kuzungumza chochote Napenda kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo limefanikiwa ni kwakupitia yeye aliye Muweza wa yote, Pili nawashukuru Watanzania wote karibu kila nyanja kwa kuonyesha ushirikiano wao kwa Mkubwa na wanawe mpaka kufikia hapa hii leo.
Mkubwa na Wanawe kwa kuungana na kampuni Mpya ambayo inajishughulisha na uuzaji na ununuaji wa vifaa mbalimbali katika mtandao High Class Look, Imeamua kutoa kidogo walichojaliwa kwa jamii kwa msimu huu wa sikuku.
High Class Look na Mkubwa na Wanawe waliweza kutembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala Maji Matitu kijulikanacho kama Hisani na kutoa misaada mbambali ikiwa pamoja na vyakula na mahitaji mengine madomadogo.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe Saidi Fella amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo kwani yeye pia ni yatima amepoteza wazazi wake wote wawili lakini pia pesa nyingi ambazo wanazipata kupitia show zao ni wale wale wazazi watoto hao walipo kuwa hai walikua wanahudulia matamasha yao na sivibaya leo tukiwakumbuka watoto wao.
Kwa upande mwingine Saidi Fella amewaomba watu wengine ambao wanajiweza na kuweza kutoa msaada wajitokeze kusaidia kwani bado watoto hao wanamaitaji na sisi wengine ni yatima watarajiwa.
Kwa upande wa mmiliki wa kituo hicho Bi Hidaya amesema kuwa changamoto bado ziko nyingi sana kituoni hapo, ya kwanza ikiwa nyumba kwani wamepanga na nyumba ndogo na watoto wako zaidi ya 50, lakini pia chakula na pesa karo kwa watoto wanaosoma shule
Toka ianzishwe Yamoto Band leo leo ni siku ya furaha kwetu kusheherekea Mwaka mmoja ambao umefanyika kuwa na mafaanikio mengi makubwa, moja kati ya mafanikio hayo ni kuuza kazi zetu kweye mtandao na kukuletea kokote ulipo mpaka majumbani
Nakwa hiki kidogo tulichokipata sisi ukijumuisha na furaha tuliyo nayo ya kutimiza mwaka mmoja tumeona nibora tugawane na wenzetu ambao ni wahitaji haswa kwa msimu huu wa sikukuu kama tulivyozoea kufanya toka kipindi chanyuma kwani hawa ni sehemu yetu kama wanajamii wenzetu..
na kwawale wapenzi na washabiki wa Yamoto Band tupo tayari kukupatia kilichobora zaidi endapo utahitaji kazi zetu wasiliana nasi utakuletea mpka nyumbani kwako
Asante
No comments: